IEBC yasema uchaguzi lazima ufanyike

Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini imewahakikishia wakenya kuwa marudio ya uchaguzi wa urais yatafanyika kama ilivyopangwa licha ya kukwama kwa mazungumzo kati yake na wawakilishi wa muungano wa NASA na chama cha Jubilee.

Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati amepeana hakikisho hilo baada ya wawakilishi wa muungano wa NASA kuondoka katika kikao cha leo na kulazimu kusitishwa kwani IEBC haingeweza kujadiliana na Jubilee pekee.

Kwenye taarifa yake baada ya kusitishwa wka kikao hicho Chebukati amegadhabishwa na misimamo mikali kati ya wawakilishi wa pande hizo mbili huku akitoa wito wa vinara wenyewe kutilia maanani kufika wenyewe katika vikao vyengine.

Amesema kuwa pande husika zilisababisha kusitishwa kwa kikao hicho sababu ikiwa ni mswada wa mabadiliko wa sheria za uchaguzi ambao kuna uwezekano wa kuathiri matayarisho ya uchaguzi.

Mwisho

Total Views: 222 ,