IEBC Kuendeleza Usajili wa Kura

Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC inatarajiwa kuanza usajili endelevu wa wapiga kura kuanzia mwezi ujao.

Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati alisema shughuli hiyo inalenga kuongeza kwa asilimia tatu kura mimiloni 19.6 zilizosajiliwa kufikia mwezi Juni mwaka ujao.

Akiongea wakati wa baraza la wasimamizi 47 wa uchaguzi na maafisa wakuu kuhusu mipango Chebukati alisema shughuli hiyo ni hitaji la kisheria linalofaa kutekelezwa.

Total Views: 124 ,