Idara ya Polisi yawakataza wafuasi wa NASA kumlaki Raila katika uwanja wa JKIA

Inspekta Generali wa polisi Joseph Boinnet amesema kuwa hakuna mfuasi wa muungano wa NASA atakayeruhusiwa kumlaki kinara wa muungano huo Raila Odinga katika maeneo ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.

Kulingana na Boinnet maeneo ya uwanja huo yanalindwa na kwamba ni wasafiri na watu walio na ruhusa ya kuingia maeneo hayo pekee watakaoruhusiwa kama vile tu siku nyengine ambapo kila mtu sharti apitie ukaguzi wa kiusalama.

Amesema kuwa umati huenda ukatatiza mikakati ya kiusalama kwa abiria,wafanyikazi na watumizi wengine wa uwanja huo mkubwa zaidi katika eneo la Afrika Mashariki ikitiliwa maanani wingi wa shughuli zake.

Viongozi wa NASA wakiongozwa na Seneta James Orengo walitoa wito kwa wafuasi wao kuelekea katika uwanja huo wa ndege ili kumpokea Raila atakayekuwa akiwasili ijumaa juma hili kutoka kwa ziara nchini Marekani na Uingereza.

Mwisho

Total Views: 234 ,