Idadi ya maafa yanayotokana na athari za mvua yaongezeka Mombasa

Idadi ya watu waliofariki kufuatia mafuriko ya mvua iliyoshuhudiwa hapa Mombasa imeongezeka hadi tisa kufuatia kuripotiwa kwa vifo vya watu watatu.

Wawili ya waathiriwa hao walifariki katika eneo la Mikindani baada ya nyumba yao kuangukiwa na ukuta huku kamanda wa polisi eneo la changamwe Peter Omanwa akidhibitisha kuwa baba na bintiye walifariki huku mama akijeruhiwa vibaya.

Muathiriwa wa tatu alifariki katika wadi ya Junda eneo bunge la kisauni ambapo mzee wa mtaa Cyphus Karisa amedhibitisha kuwa mwendazake alikuwa akitembea kwa maji hayo ya mafuriko wakati mvua ilipokuwa ikiendelea kunyesha.

Mwisho

Total Views: 393 ,