Hart Aelekea Italia

Kipa Joe Hart kusafiri leo kuelekea Italia kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu kabla ya kujiunga na klabu ya Torino inayoshiriki ligi ya serie A.

Hart atajiunga na klabu hiyo kwa mkopo iwapo atapita uchunguzi huo wa kimatibabu.
Hart mwenye umri wa miaka 29 amepewa ruhusa na shirikisho la soka nchini Uingereza FA, kuondoka katika kambi ya timu ya taifa ya Uingereza na kuelekea Italia.

Nafasi yake katika klabu ya Mancity ilikuwa ati ati baada ya kuwasili kwa kipa Claudio Bravo hatua inayomfanya kusalia nambari 3 baada ya Caballero na Bravo.

Total Views: 328 ,