Harambee Stars yashuka viwango vya Fifa

Timu ya taifa ya soka Harambee Stars imeshuka hadi nafasi ya 110 katika orodha ya viwango vya FIFA kwa taifa bora kwa soka duniani kutoka nafasi ya 105.
Katika kanda ya CECAFA Uganda inaongoza ikiwa katika nafasi ya 74 huku mataifa ya Rwanda, Sudan, Tanzania, Ethiopia, Burundi, pamoja na Sudan kusini zikifuata nyuma ya Kenya.
Kenya ilipoteza mechi za kirafiki majuzi ambapo ilitingwa 3-2 na jamhuri ya Afrika ya kati, sawa na kutoka sare ya 2-2 na visiwa vya Comoros.
Ujerumani inaongoza duniani licha ya kutingwa na Brazil katika mechi ya kirafiki mwezi jana ambapo brazil,ubelgiji,ureno , argentina zinashikilia nafasi 5 za kwanza.
Uswizi , Ufaransa , uhispania,chile na Poland zinafuatana kutoka nafaSI YA 6-10.
Tunisia inayohorodheshwa bora afrika imepanda jhadi nafasi ya 14

Total Views: 115 ,