GrandPa records ndio lebel kubwa Kenya

GrandPa

Kenya pamekuwa na lebel kubwa kama Mandugu digital, Calif records, Ogopa Djs, Sub-Sahara, Homeboyz , lebel ya Tedd Josia ‘Blue Zebra’ na kwa sasa kuna Grandpa Records.

Grandpa records ni miongoni mwa lebel kubwa Kenya sasa kutokana na sababu hizi

1. Grandpa imetoa nyimbo kali zaidi ya 10 kila mwaka ndani ya miaka mitano,

Grandpa imemudu kutoa nyimbo zilizofanya vizuri kwenye radio na tv kila mwezi ndani ya miaka sita ya kazi zake za muziki, wasanii kama Kenrazy ,Sosun ndio wanashikilia lebel hio.

Refigah Boss wa GrandPa

2. Boss wa lebel Yusuf Noah aka Refigah anauzoefu wa zaidi ya miaka 20 kwenye muziki Kenya ikiwa alianza kama msanii.

Hichi kitu kimeweza kumfanya aweze kupambana na mabosi wa lebel kubwa kama Musyoka na Tedd Josiah

Refigah hatengenezi muziki ila anajua cha kutengeneza kwenye soko la muziki.

Kenrazy Msanii wa Grandpa

3. Mpango wa GrandPa sio kushika Kenya tu ila Afrika mashariki kwa ujumla.

Tofauti na lebel zingine Grandpa haifanyi kazi ili ibaki juu inafnya kazi ili kupanuka zaidi na kuwa na soko kubwa la kuuza kazi zake. Kwa sasa Grandpa wapo Uganda wanasajili vipaji vipya.

Refigah alikuwa Southern Sudan, Rwanda na Burundi akisaka vipaji.

Sosuun Msanii wa Grandpa

4. Style ya wasanii wa Grandpa imewachukua wakenya wengi.

Wasanii wa Grandpa wamekaa mbali na style za kuimba kama Genge, Jipuka na Boomba na kubuni style yao peke kama unavyowasikia kwenye wimbo wa ‘Dawa ya moto ni moto”.

Visitaa Msanii wa Grandpa

Msanii DNA alijitoa Grandpa mwaka jana na kufeli sana kimuziki huku lebel yake ikibaki kuwa juu.

Wimbo mwingine mkubwa wa GrandPa ni wa Sosuun ‘Sura ya kazi’.

Total Views: 734 ,