Gor Yasema Thiago haondoki

Mwenyekiti wa klabu ya kogallo Ambrose Rachier amethibitisha kuwa mshambulizi kutokea taifa la Brazil Thiago da Silva atasalia ndani ya klabu hiyo kwa miezi mingine sita akifanyiwa majaribio na kisha kujiunga na Gor iwapo fomu yakle itakubalika.

Silva alitua Kenya mapema mwezi huu na baada ya wiki chache inaonekana kana kwamba fomu yake haijaridhisha wasimamizi wa klabu hiyo huku pia ikitarajiwa kutangaza msimamo kuhusu mganda Meddie Kagere ambaye amekuwa akifanya mazoezi na klabu hiyo.

Total Views: 345 ,