Taita Taveta:Gavana Samboja awaonya polisi dhidi ya kuwaachilia washukiwa kiholela

Gavana wa kaunti ya Taita Taveta Granton Samboja ametofautiana na hatua ya polisi kuwaachilia baadhi ya washukiwa wanaohusishwa na wizi na mauaji ya wahudumu wa boda boda katika kaunti hiyo.

Gavana Samboja anadai kuwa hatua hiyo inachangia ongezeko la visa hivyo hivi punde ikiwa kuachiliwa kwa washukiwa wawili licha ya kupatikana na mali na stakabadhi zinazodaiwa kuwa za muhudumu aliyeuwawa mwaka jana.

Huku hayo yakijiri viongozi wa kisiasa sawa na wa kidini katika kaunti ya taita Taveta wanashinikiza kuhamishwa kwa baadhi ya maafisa wa polisi mjini Voi kwa madai kuwa wanashirikiana na wahalifu.

Hata hivyo polisi wamepinga madai hayo wakisisitiza kuwa kuachiliwa kwa washukiwa kunafuatia kukosekana kwa ushahidi ambapo mtu hulazimika kuachiliwa kwa mujibu wa sheria.

Mwisho

Total Views: 209 ,