Gavana Kivutha Kibwana akamatwe,asema Kisoi

Kisoi Mbooni mpMbunge wa Mbooni Kisoi Munyao na mwenzake wa Kaiti Richard Makenga kwa sasa wanataka kukamatwa kwa Gavana wa Makueni Prof Kivutha Kibwana kuhusiana na mkasa wa moto uliounguza majengo ya bunge la kaunti hiyo jumatatu.

Wakiwahutubia wanahabari nje ya majengo ya bunge mapema leo,wawili hao wamedai kuwa Gavana Kibwana ana taarifa muhimu zinazoweza kusaidia pakubwa katika uchunguzi wa kubainisha chanzo cha mkasa huo.

Wamedai kuwa Kibwana alichagua kutowapa maafisa wa usalama taarifa kuhusu mkasa huo hatua ambayo ni kinyume dhidi ya majukumu yake ya kuchunga rasilimali za kaunti kwa mujibu wa sheria.

Wanasema kuwa ni jambo la kusitikisha kuona kuwa kaunti ya makueni inakosa magari ya zima moto licha ya kutengwa kwa pesa za ununuzi wa vifaa hivyo kwenye bajeti ya mwaka jana huku moto huo ukiteketeza ofisi ya spika,karani na bunge la kaunti hiyo.

Mwisho

Total Views: 370 ,