GAVANA KINGI NA UFISADI

Gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Kingi ameihimiza serikali kutenga pesa zaidi kwa kamati za kupambana na ufisadi katika ngazi ya kaunti ili kufanikisha vita dhidi ya ufisadi.

Gavana huyo amesema raslimali zinazotengewa kamati hizo hazitoshi kuziwezesha kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Kingi alikuwa akiongea alipokutana na wanachama wa kamati hiyo.

Alisema vita dhidi ya ufisadi vitashindwa kupitia kampeni ya kitaifa inayotilia mkazo umuhimu wa uadilifu.

Picha kwa hisani.

Total Views: 20 ,