Gavana Kingi na Michezo,Kilifi

KINGI KILIFI MICHEZOGavana wa kaunti ya Kilifi Amason Kingi amesema kwamba mfumo mpya wa elimu ambao unanuia kuanzishwa hivi karibuni utasaidia wanafunzi kukuza  talanta na pia kiwango cha elimu nchini.

Akizungumza katika ofisi yake pale alipokuwa akiwakabidhi rasmi bendera na jezi mpya za michezo wanafunzi wa kaunti ya kilifi wanaoshiriki katika michezo ya mikoa huko kwale, Kingi amesema kwamba ni muhimu kukuza talanta katika vijana hao.

Vilevile, amesema kwamba nidhamu katika michezo hii lazima idumishwe kwani ndio chanzo cha mafanikio katika michezo na hata masomo yao kwa jumla.

Kingi amesema kwamba kujihusisha kwa wanafunzi katika michezo kutawaokoa vijana wengi katika kushiriki kwenye tabia potofu ikiwemo ulanguzi wa dawa za kulevya na mimba za mapema.

Wanafunzi hao kutoka kaunti ya Kilifi wanaelekea Kwale kwa ajili ya michezo ya Mikoa ikiwemo soka, mpira wa nyavu, pete na mpira wa mikono kwa makundi ya wasichana na wavulana.

Mwisho

Total Views: 522 ,