Raila awasili Malindi kwa mkutano wa Amani

Kinara wa CORD Raila Odinga amewasili mjini Malindi tayari kwa mkutano wa amani unaotarajiwa kufanyika katika uwanja wa Cleopatra kwa lengo la kutuliza joto la kisiasa linaloshuhudiwa nchini.

Mkutano huu unajiri saa chache kabla ya mazishi ya muwakilishi wa wadi mteule Grace Chihanga katika eneo la Kambe kaunti ndogo ya Kaloleni kesho jumamosi ambapo Raila ni miongoni mwa viongozi watakaohudhuria.

Viongozi wengine walioandamana na Raila ni seneta Johnstone Muthama,Stewart Madzayo,James Orengo na wabunge Junet Mohamed,Aisha Jumwa na Florence Mutua.

Mwisho

Total Views: 401 ,