Gavana Awiti apoteza kiti chake Homa Bay

Gavana wa Homa Bay Cyprian Awiti ni wa hivi punde kupoteza kiti chake kufuatia uamuzi wa mahakama ya rufaa uliodumisha uamuzi wa awali wa mahakama ya juu uliobatilisha uchaguzi wake.

Uamuzi wa jopo la majaji watatu uliosomwa na jaji Fatuma Sichale umebaini kuwa kulikuwa na ushahidi wa kutosha wa kuonyesha kuwa uchaguzi wa Awiti haukuwa wazi na huru kama ilivyoamuliwa awali na mahakama ya juu.

Aliyekuwa mbunge wa Kasipul Oyugi Magwanga ambaye aliibuka wa pili kwenye uchaguzi wa ugavana mwezi agosti mwaka jana alikuwa ameshinda kwenye rufaa ya kupinga uchaguzi huo ila Awiti akakata rufaa.

Kwa sasa mahakama imemuagiza Awiti na tume huru ya uchaguzi na mipaka kumlipa Oyugi shilingi milioni nne na mbili mtawalia kama garama za kesi huku IEBC pia ikiagizwa kuandaa uchaguzi mdogo.

Mwisho

Total Views: 281 ,