EACC ni bora Barani Afrika yasema Jumuiya ya madola

 

Tume ya maadili na makabiliano dhidi ya ufisadi nchini EACC imeorodheshwa ya kwanza  Barani Afrika mbele ya tume nyingine kumi na saba.

EACC imeorodheshwa bora zaidi katika kushughulikia na kusimamia ushahidi kuhusu ufisadi ikilinganishwa na bodi nyingine katika mataifa kumi na saba barani.

Pia imeorodheshwa ya kwanza katika kuzingatia kiapo cha afisi ,kanuni za maadili ,taarifa za majukumu na mfumo wa sera na taratibu.

Hatua hiyo inajiri kufuatia utafiti uliofanywa kati ya mwezi Juni mwaka 2015 na mwezi huo mwaka jana na  afisi ya Jumuiya ya madola na ya umoja wa mataifa kuhusu dawa za kulevya na uhalifu.

Total Views: 275 ,