Duale, awataka NASA kutekeleza vitisho vya kususia uchaguzi

Kiongozi wa wengi katika bunge la taifa Aden Duale ameuonya muungano wa NASA dhidi ya kutekeleza vitisho vyake vya kususia uchaguzi wa Agosti akiitaja hatua hiyo kama iliyopitwa na wakati.

Akizungumza mjini Garissa Duale amesema kuwa zama za kutishia taasisi na washirika wengine zilikwisha huku akisisitiza kuwa muungano huo umetambua kuwa utashindwa kwenye uchaguzi huo ndio maana unatafuta sababu ya kupinga matokeo hayo.

Muungano wa NASA umetishia kushinikiza maandamano kote nchini sawia na kususia uchaguzi wa Agosti iwapo mahakama itabatilisha uamuzi wa kutaka matokeo ya kura za urais kutangazwa katika kiwango cha eneo bunge.

Mwisho

Total Views: 292 ,