Divock amezewa mate na Athletico Madrid

Mbelgiji mwenye asili ya Kikenya Divock Origi anayewajibikia klabu ya Liverpool ametajwa kuwa mmoja wa sajili wanaopigiwa upato na mkufunzi Diego Simone anaefunza klabu ya Athletico Madrid, baada yake kukosa huduma za diego costa kutokea klabu ya Chelsea pamoja na Gonzalo Higuain kutokea klabu ya Napoli.

Aidha klabu hiyo inapania kupata sajili hizo kupata mjazo wa Jackson Martinez na Origi anaonekana kuwa kifaa kamili,huku pia akitaka sajili za Kevin Gameiro kutokea klabu ya Seville,Rumelu Lukaku kutokea Everton, pamoja na Edison Carvan kutokea klabu ya ya PSG.

Total Views: 386 ,