Dimba la CECAFA kuandaliwa Kenya

CECAFA imethibitisha kuwa taifa la Kenya litakuwa mwenyeji wa dimba la CECAFA Senior Challenge pamoja na lile la Kagame mnamo mwezi disemba mwaka huu haya yakijiri baada ya kukosena kwa nchi mwenyeji wa michuano hiyo.

Dimba la Kagame lingefanyika kati ya mwezi juni na julai mwaka huu ila kukakosekana nchi mwenyeji, haya yamethibitishwa na katibu wa CECAFA Nicholas Musonye.

Mara ya mwisho Kenya kuwa mwenyeji wa dimba la Kagame ilikuwa mnamo mwaka 2001 ambapo klabu ya wanamvinyo Tusker Fc iliibuka kidedea.

Total Views: 382 ,