Daktari Swizerland Asubiri Uamuzi wa Mahakama Baada ya Kumua Bintiye

Mwanamke mmoja Mtaalamu wa kufanya operesheni  huko Swizerland  ameuupuka kufungwa kutokana na kosa la kumuweka  msichana wake karatasi ya nylon  aliyekuwa na saratani na kisha kukosa hewa na kufariki.

Jaji anayeshughulikia kesi hiyo ametaja kesi hiyo kama ngumu sana kuamua kwa kuwa daktari huyo  hujawahi kutekeleza uhalifu na  pia wanachunguza sababu zilizosababisha kumuua msichana huyo mwenye umri wa miaka 14.

Daktari huyo anadai kuwa mwanawe alimuambia mara nyingi kuwa alikuwa anataka kufa  kwa sababu hangesubiri kifo kwa kuwa hakukuwa na sababu yoyote ya kuishi.

Anasema kuwa hali hiyo ilimsukuma kumuua bintiye na madai hayo yametupiliwa mbali na babake anayesema hakuna siku bintiye alitamka neno moja la kutaka kujiua.

Pia mshukiwa  aliliezea jinsi alivyokuwa akimeza dawa alizokuwa anawapa wagonjwa wake kwa matumaini kuwa wangekufa pamoja.

Total Views: 50 ,