Conte anafaa kusalia chelsea – Marcel Desaily

Kiranja wa zamani wa klabu cha Chelsea Marcel desaily amesema mmiliki wa klabu cha Chelsea Roman Abromovich sharti ambakishe klabuni humo mkufunzi Antonio conte na badala yake kuuza baadhi ya wachezaji.

Desaily amesisitiza masaibu ya Chelsea kwa sasa haifai kumlaumu mkufunzi bali ni utepetevu wa klabu kizima na kwamba mkufunzi huyo hakupewa fursa ya kusajili wachezaji aliokusudia kuimarisha zaidi kikosi msimu huu.

Iwapo Conte ataondoka itakuwa mkufunzi wa 13 tangu Abromovich kunua klabu hicho..

Total Views: 180 ,