Collins Adede

COLLINS ADEDE

Ni Mwanahabari mtangazazi wa kipindi cha Uchambuzi wa magazeti na vile vile ni rubani wa kipindi cha Reggaeblast akifahamika kama “Ras Colo” kila siku ya jumapili.
Shabiki huyo wa AFC yaani AFC Leopards na pia Arsenal alipata elimu yake Mombasa Polytechinic kwa sasa ikifahamika kama Techinical University.
Kando na Kubobea katika utangazaji ni msoma habari, mtayarishi wa matangazo ya biashara na pia vipindi na mahanjamu ambayo huvutia redioni na kukipa kituo sura fulani inayobainishwa na vituo vingine kila unaposikiza.
Kando na kuwa mpishi shupavu wa Pilau, anapendelea mziki wa Reggae na Rhumba.
Amecheza mchezo wa Voliboli japo taaluma ya uwanahabari iliteka hisia zake na pia ni mkulima shupavu.
Kutana naye kila siku ya jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa 5AM hadi 9AM kisha kila jumapili kuanzia saa 1Pm hadi 5PM kupata burudani.
Ukurasa wake wa Twitter ni @colynsadede ama Colyns Liberty Adede kwenye Facebook.

Total Views: 1278 ,