Clemence Jilo

Mashabiki wake wanampenda kwa ustadi wake wa kuendesha kipindi cha Bango kinachokukujia kila siku ya Jumamosi saa tatu hadi saa saba. Anajulikana kama queen of bango Dj tausi .Pia ni mtetezi wa wanawake na hapendi kuona msichana yeyote akidhulumiwa.

anasimamia kutayarisha matangazo ya kibiashara ya wateja. Anasema ni sharti uwe mwenye maarifa na mbunifu sana kufanya kazi hiyo.

Hauwezi kumtenganisha na mambo ya Pwani hasa harusi. Na mara nyingi huwa MC wa kukata keki wakati wa sherehe za harusi.

Ni mama wa wavula wawili, kiongozi wa vyama mbali mbali vya maendeleo vya kina mama na pia mwalimu wa Sunday School.

Alisomea uanahabari katika chuo kikuu cha Moi.

Total Views: 995 ,