City Stars yapata Mkufunzi Mpya

Siku chache baada ya kuondoka kwa mkufunzi Bobby Ogola klabuni City stars kujiunga na klabu ya Muhoroni,stars tayari mkufunzi mwingine ameonekana akinoa kikosi hicho.

Mkufunzi huyo ambaye amefahamika kwa jina la Richard anatarajiwa kuchukuwa nafasi ya Ogolla huku mwenyekiti wa klabu hiyo Peter Jabuya akisema kuwa hatma kamili itajulikana hivi karibuni.

Stars imekuwa ikizongwa na matatizo ya kifedha kwa siku za hivi karibuni hatua iliyopelekea baadhi ya wachezaji nyota kuihama klabu hiyo

Total Views: 333 ,