Chris Brown akatazwa kumuona Mpenziwe

Itakuwa vigumu, kwa Chris Brown msanii mwenye sifa tele kumutupia jicho mpenziwe wa zamani baada ya mahakama kumzuia.

Karrueche Tran anadai kwamba alimtishia kumuua mwezi Disemba na kufichua kuwa alijaribu kumpiga tumboni na kumsukuma kwenye ngazi japo hakupiga ripoti kwa polisi.

Kulingana na shirika la BBC, mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 28 amemshutumu mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kwa kuwaelezea watu kadhaa kuwa angemua .

Wawili hao walikuwa wapenzi  mwaka 2015 lakini wakawachana baada ya miezi kadhaa.

Total Views: 411 ,