Chiloba akata rufaa dhidi ya uamuzi wa IEBC wa kumuachisha kazi

Afisa mkuu mtendaji wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC Ezra Chiloba amewasilisha rufaa katika mahakama ya leba akipinga uamuzi wa mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati wa kumsimamisha kazi.

Kwenye rufaa hiyo,Chiloba anasema kuwa hakupewa fursa ya kujitetea kabla ya kupewa likizo ya lazima huku akiwaorodhesha makamishna Abdi Guliye na Boya Molu kama wahusika kwenye rufaa hiyo.

Kwa sasa Chiloba anataka mahakama kupeana maagizo ya mda ya kumruhusu kurejea kazini sawia na kufichuliwa kwa madai ya kutowajibika katika maswala ya ununuzi yanayoibuliwa dhidi yake.

Hatua hii inajiri baada ya Chebukati na Makamishna wengine kuamua kumpa afisa huyo likizo ya lazima ya mda wa miezi mitatu ili kuruhusu uchunguzi huru kufanyika dhidi ya madai ya kutowajibika kwa Chiloba wakati wa ununuzi wa vifaa vya tume hiyo.

Mwisho

Total Views: 162 ,