CHANGAMOTO YA MTAALA MPYA TAITA

Sekta ya elimu ya chekechea kaunti ya Taita Taveta bado inakumbwa na changamoto kuhusiana na mtaala mpya kutokana na ukosefu wa vitabu  vya kuwaongoza wanafunzi.

Sekta hiyo ya elimu inadai  kuwa mtaala huo mpya wa elimu umekanganya pakubwa wanafunzi kutokana  na kwamba wengi hawajajua kusoma wala  kuandika.

Akizungumza huko mbololo katika eneo bunge la voi,msimamizi wa elimu ya chekechea katika eneo hilo Faith Mlamba, amedokeza kuwa kumekuwa na lalama kutoka kwa wazazi na walimu kwani asilimia kubwa ya watoto hawajui kusoma na kuandika chini ya mtaala huo mpya.

Anadai  mtaala wa sasa haumpi mwanafuzi nafasi ya kushindana na wengine ikilinganishwa na mtaaala uliopita.

Hata hivyo waalimu wa chekechea wameitaka serikali ya kaunti kwa ushirikiano na serikali ya kitaifa kushirikiana kwa lengo la kuhakikisha vitabu vya kutoa mwongozo vimepatikana kwa wingi kwa lengo la kufanikisha mtaala huo.

Picha kwa hisani.

 

Total Views: 61 ,