CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA BANDARI KUELEKA MAHAKAMANI

Chama cha wafanyakazi wa Bandari ya Mombasa kwa ushirikiano na shirika la kutetea haki za kibinadamu la MUHURI linatarajiwa kuelekea mahakamani leo kupinga mpango wa serikali kukodi sehemu ya makasha ya mizigo almaarufu Container Terminal 2 bandarini.

Katibu wa chama hicho Simon Sang anadai kwamba hatua hiyo ni ya kuizuia serikali kukodi sehemu hiyo kwa kampuni ya kitaifa kuhusu uchukuzi wa Meli ikizingatiwa kwamba inakiuka katiba ya nchi.

Sang amesisitiza kwamba chama hicho hakitakubali zaidi ya nafasi za ajira elfu nne ambazo zinastahili kuwafaidi wakaazi wa pwani kupotezwa kufuatia hatua hiyo ya serikali.

picha hisani

 

Total Views: 16 ,