CDF ni pesa za umma asema Awiti

Mbunge wa Nyali Hezron Awiti ametofautiana vikali na viongozi wanaoiita kwa majina yao miradi iliyotekelezwa kwa pesa za umma akisema kuwa si sawa ikizingatiwa kuwa sio pesa zao zilizotumika.

Akizungumza alipozuru baadhi ya miradi iliyotekelezwa kupitia pesa za ustawi wa eneo bunge la Nyali, Awiti amesema kuwa ni wakati sasa kwa wanasiasa kutotumia pesa za umma kujifanyia kampeini.

Amedokeza kuwa tayari amepata mfadhili kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha mafunzo katika eneo bunge la Nyali, mradi unaotarajiwa kung’oa nanga kuanzia mwaka ujao kwa manufaa ya wakaazi wa eneo bunge hilo.

Kadhalka ametoa wito kwa wakaazi wa kaunti ya Mombasa kumuunga mkono kwenye azma yake ya kugombea ugavana mwaka ujao akidai kuwa ana uwezo wa kutekeleza miradi zaidi ya maendeleo kuliko ile inayoonekana kwa sasa.

Mwisho

Total Views: 419 ,