BUSTANI YA MAMA NGINA KUKAMILIKA AGOSTI

Mradi uliogharimu shillingi millioni 460 kukarabati bustani la mama ngina, uliozinduliwa na rais Uhuru Kenyatta tarehe 7 mwezi Januari, utakabidhiwa kwa serikali tarehe 15 mwezi Agosti mwaka huu.

Akizungumza na wanahabari baada ya kuzuru eneo hilo waziri wa utalii Najib Balala, amesema kuwa tayari mwanakandarasi amewahakikishia kwamba mradi huo utakua umekamilika ifikapo tarehe 15 mwezi Agosti mwaka huu na kisha kukabidhiwa kamati ya kitaifa kuhusu matamasha ili eneo hilo litumike kwa sherehe za Mashujaa mwaka huu.

Hata hivyo mradi huo uliojengwa kwenye ardhi ya ekari 26 ulitakiwa kukamilika tarehe 31 mwezi Mei.

picha hisia

Total Views: 22 ,