Bungeni:Si kweli ni uvumi tu, wasema wabunge kuhusu kiinua mgongo

Wabunge wamepinga madai kuwa wanapania kujizawidi kiinua mgongo cha hadi shilingi bilioni 2.5.

Kauli yao inajiri kufuatia madai kuwa wamekuwa wakishinikiza kupewa fedha hizo ambapo kila mbunge ataenda nyumbani na shilingi milioni 6.2 kama fidia kutokana na kuwa mda wao wa kuhudumu utakamilika miezi minane mapema kufuatia uchaguzi mkuu.

Wakiongozwa na kiongozi wa wengi katika bunge la taifa Aden Duale,wabunge hao wanaonekana kuchukizwa na taarifa iliyochapishwa kwenye magazeti ya humu nchini ikidai kuwa wamepanga njama ya kujilipa mshahara kwa kazi ambayo haijatekelezwa.

Mwisho

Total Views: 306 ,