Bunge latafuta suluhu dhidi ya mzozo wa IEBC

Kamati ya bunge kuhusu haki na maswala ya sheria imepangiwa kukutana na ile ya usimamizi wa utekelezaji wa katiba ili kukubaliana kuhusu njia mwafaka ya kufanyia mabadiliko tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC.

Kwenye mkutano ulioitishwa na mbunge wa Mukurweini Kabado wa Kabando na mwenzake wa Tarbaj Ibrahim Elmi wanapania pia kutumia kikao cha kesho kutafuta mbinu za kushinikiza umoja miongoni mwa wakenya.

Tayari kamati hiyo ya sheria imeonekana kuunga mkono kubuniwa kwa jopo la uteuzi wa makamishna wapya licha ya bunge kusisitiza haja ya kuweko kwa shera mpya itakayobaini wale watakaohudumu kwa tume hiyo.

Wale wanaounga mkono wanahoji kuwa miungano miwili ya kisiasa inastahili kupewa fursa ya kuchagua watu wawili kila muungano huku wengine watatu wakichaguliwa na tume ya huduma za umma huku jopo la uteuzi likiwachagua makamishna tisa.

Mwisho

Total Views: 388 ,