Bunge Larajelea Vikao Vyake Leo

Bunge la taifa  linarejelea vikao vyake leo huku  mchakato wa kutaka kujaza nafasi ya inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinnet ambaye mda wake wa kuhudumu wa miaka minne unakamilika mwezi Machi mwaka huu ukiwa miongoni mwa ajenda kuu.

Kulingana na kiongozi wa wengi Aden Duale  kutafuta mrithi anayefaa wa inspekta huyo mkuu ni miongoni mwa ajenda muhimu za  vikao vya leo.

Hata hivyo kabla hatua hiyo wabunge watazingatia majina ya watu walioteuliwa kuhudumu katika tume ya huduma za polisi.

Total Views: 82 ,