Bunge la Kitaifa Kurejelea Vikao Leo

Bunge  la taifa litarejelea vikao vyake leo  mchana baada ya  likizo ya mwezi mmoja ,kwa mara ya kwanza tangu wabunge walipoidhinisha mswada wa fedha wa 2018 ulioibua mseto wa hisia kutoka kwa viongozi na umma..

Kikao cha leo kitajumuisha mda wa masuali ambapo wabunge watapewa fursa ya kuuliza masuali mafupi yatakayohitaji mawaziri kutoa majibu.

Kamati ya bunge kuhusu taratibu na kanuni inayoongozwa na spika Justin Muturi inasema itapunguza mda unaotumiwa na wabunge kujadili majibu yanayotolewa na wenyeviti wa kamati za bunge.

Total Views: 114 ,