BOZI KUMI NA SITA ZA KUSIMAMIA ARDHI TAYARI

 

Shughuli zote za ardhi kote nchini sasa zinaweza kurejelewa baada ya wizara ya ardhi kuanza shughuli za kuunda upya bodi  simamizi za ardhi.

Bodi hizo zilivunjwa mwezi Eprili na waziri wa ardhi Prof.Jacob Kaimenyi,ambaye sasa ametangaza kwamba bodi mpya za ardhi zimeundwa katika kaunti 16 katiya 47 na kwamba majina ya wanachama yamechapishwa kwenye gazeti la serikali.

Kaunti ambazo kufikia sasa zina bodi mpya  za ardhi ni pamoja na Kilifi,Taita-Taveta,Kwale,Meru, Samburu, Embu, Kericho, Nyeri, Kirinyaga, Kisumu, Machakos, Elgeyo-Marakwet, Narok, West Pokot, Murang’a na Vihiga.

Ameongeza kwamba wizara hiyo itaendelea kuchapisha bodi zaidi mara tu kaunti zilizosalia  zitakapokubaliana na  sheria na taratibu zilizowekwa.

Hatua hiyo sasa inauruhusu umma kujihusisha na  shughuli za ardhi ambazo zilikua zimekwama kwa mda wa zaidi ya miezi miwili.

Total Views: 340 ,