Bishara Aden

BISHARA ADEN

Tofauti na wanawake wengine ambao hawapendi kutaja umri wao,  yeye anajinaki kuzaliwa mwaka 1989 , amejaliwa umbo la kupagawisha na urembo pia kapewa.

Kilichomuingia katika damu yake zaidi ni mziki wa Taarab ambao umempelekea kuendesha kipindi cha Taarab “KWA RAHA ZANGU”.

Anapenda, kazi za nyumbani zaidi ikiwemo kupika, kufua, kusafisha nyumba ila hapendi kuoka yaani “BAKING”.

Mbali na utangazaji, ni mwigizaji wa filamu tofauti ikiwemo vipindi ya runinga vya humu nchini na mwenye mipasho ya ajabu ya kukuacha kinywa wazi.

Mtoto huyu wa Mombasani huenzi sana msemo huu anapokuwa kazini – “Napatikana papa hapa Pwani Fm kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa mida ya maankuli saa Sita hadi saa nane mchana.”

 

Total Views: 1755 ,