BIASHARA YA VINYAGO KUNOGA

Huenda wafanyabiashara wa kuchonga vinyago katika karakana ya Akamba Handcraft katika eneo bunge la Changamwe wakatekeleza biashara yao kwa masaa ishirini na nne licha ya ukosefu wa umeme.

Hatua hiyo inajiri baada ya serikali ya kaunti ya Mombasa kukabidhi karakana hiyo  Jenereta ya kisasa ambayo itawahudumia wakati wowote.

Akiongea na wanahabari afisa wa mambo ya utamaduni na sanaa katika kaunti ya Mombasa Khamis Juma Kurichwa amesema Jenereta hiyo itawasaidia pakubwa hasa wakati umeme utakapokuwa na shida.

Wakati huo huo Kurichwa amesema kwamba wamepanga kuweka mikakati ya kuboresha biashara ya vinyago ndani na nje ya nchi kidijitali baada ya kujumuika na vitengo mbali mbali katika kaunti hiyo.

Picha kwa hisani.

Total Views: 27 ,