Bandari yamwachilia Karani kwa mkopo

Mchezaji wa klabu ya Bandari Meshack Karani anatarajiwa kujiunga na klabu ya kakamega home boiz kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu.

Karani amabaye aliwahi kuchezea klabu ya chemelil sugar ameshindwa kufana katika klabu ya Bandari ambayo ni wawakilishi wa pwani na amekuwa akitafuta mwanya wa kuondoka kutafuta lishe kwingineko na sasa atakuwa mchezaji wa tatu kuondoka baada ya Edwin wafula na Bernard Mang’oli ambao wameelekeza huduma zao katika klabu ya Ingwee

Hatua yake kuondoka klabuni humo imethibitishwa na mkurugenzi wa benchi la kiufundi Edward Oduor.

Total Views: 381 ,