Bandari yalenga kuitungua Gor-mahia

Klabu cha Bandari kinapania kuwa klabu kitakachotamatisha msururu wa ushindi wa vinara na mabingwa watetezi wa ligi ya kitaifa Gor Mahia, itakapokumbana na klabu uwanjani Mbaraki hapo kesho.

Bandari, almaarufu, Dockers, wameandikisha matokeo ya kuridhisha tangu Bernard Mwalala kutwaa mikoba ya ukufunzi baada ya kuondoka kwa Ken Odhiambo akiwa tayari ameiongoza kucheza mechi 4.

Bandari italazimika kujitahidi dhidi ya Gor Mahia, ambao wanalenga kurejesha uongozi wake wa alama 16 kileleni pa ligi kuu.

Kā€™Ogallo ilitoka sare mabao mawili kwa mawili dhidi ya Nakumatt, huku ushindi wa Sofapaka wa bao moja kwa sifuri dhidi ya Ulinzi Stars ukipunguza uongozi wa Gor hadi alama 13.

Total Views: 165 ,