Balozi wa Marekani Asema Miradi ya Ajenda Nne Ni Sharti Itiliwe Maanani

Balozi wa Marekani nchini  Kenya Kyle McCarter asema hazina iliyotengwa kutekeleza miradi ya ajenda kuu za serikali haipaswi kufujwa.  

Kwenye mahojiano ya kipekee na Pwani FM, McCarter anasisitiza kuwa agenda hizo  kuu zinalenga kuwanasua wakenya wengi kutokana na matatizo yanayowakabili na haipaswi kuchukuliwa kama  mbinu ya rais Uhuru Kenyatta ya kuwacha alama atakapostaafu.

Waziri wa fedha Henry Rotich alitenga jumla ya shilingi bilioni 450 ya kufanikisha ajenda hizo kwenye makadirio ya bajeti ya mwaka 2019/2020.

Balozi huyo asema japo rais Uhuru Kenyatta amejitolea kukabiliana na ufisadi, lakini inachukuwa muda mrefu kwa washukiwa kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

 

 

Total Views: 18 ,