Balala Alaumu Ubalozi wa Marekani Kuhusiana na Ilani ya Usafiri

Waziri wa utalii Najib Balala ameulaumu ubalozi wa Marekani humu nchini kwa kile anachodai kama kulitia chumvi agizo la kuwaonya raia wake walioko nchini kuwa waangalifu kutokana na uwezekano wa mashambulizi ya kigaidi.

Balala amesistiza kuwa onyo hilo lilinuia kuwatahadharisha Wamarekani lakini sio kuwakataza kuja nchini Kenya.

Wakati huo huo Balala amewahakikishia wakenya,watalii wa humu nchini na wa kigeni kwamba Kenya iko salama.

Total Views: 56 ,