BAA LA NJAA KWALE

Wakaazi elfuĀ 45 kaunti ya Kwale wanakumbwa na baa la njaa na uhaba wa maji,kutokana na ukame unaoendelea kushudiwa eneo hilo.

Akizungumza katika eneo la Mbuguni huko Matuga,waziri wa ugatuzi Eugen Wamalwa ametoa hakikisho kuwa serikali ya kitaifa imejitolea kukabiliana na janga hilo.

Wakati huo huo Gavana wa Kwale Salim Mvurya amewataka waathiriwa kuwa wavumili,wakati serikali inapoendelea kuwashughulikia.

Wawili hao wamesema hayo kwenye shughuli ya ugavi wa chakula cha msaada inayoendelea kaunti ya Kwale.

Picha kwa Hisani

Total Views: 28 ,