Atwoli ahimiza majadiliano kati ya rais Uhuru na Raila odinga

Muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini COTU umetoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo kati ya chama cha Jubilee na muungano wa Upinzani NASA ili kutafuta suluhu dhidi ya mzozo wa kisiasa unaoikumba nchi hii.

Akizungumza na wanahabari,katibu mkuu wa COTU Francis Atwoli amemsihi rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa Upinzani Raila Odinga kukutana na kujadiliana kwa lengo la kuiepusha nchi hii dhidi ya kutumbukia katika mzozo.

Aidha Atwoli amesema kuwa muungano wa COTU uko tayari kupanga na kuitisha majadiliano hayo iwapo utaruhusiwa ukisema kuwa tayari uko na orodha ya watu mashuhuri wanaoweza kuongoza kikao hicho.

Miongoni mwa watu anaowapendekeza ni Yusuf Haji,Amos Wako,Jamleck Kamau,Dr Oburu Odinga,Abraham Kiptanui,Hassan Ole Kamwaro,Zipporah Kittony,Chris Kirubi,David Musila,Phoebe Asiyo na waziri wa zamani wa Leba Philip Masinde.

Mwisho

Total Views: 172 ,