Atwoli adai kuwa shilingi bilioni 11 za Malipo ya Uzeeni hazijulikani zilipo

Katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini COTU Francis Atwoli anadai shilingi bilioni 11 kwenye mfuko wa hazina ya malipo ya uzeeni NSSF hazijulikani zilipo.

Atwoli anadai bodi ya walinda dhamana ambayo imekua ikichunguza kashfa hiyo iliyotokea kablla ya  kuingia uongozini inapitia vikwazo kutoka  kwa baadhi ya watu binafsi wasiotaka ukweli kujulikana.

Akihutubia waandishi wa habari katika makao makuu ya COTU Atwoli amesema kwamba hatua ya kujiuzulu kwa mwenyekiti wa bodi hiyo Kariithi Murimi ilitokana na kuingiliwa na watu katika hazina ya NSSF wasiotaka uchuguzi huo kuendelea.

Sasa Atuoli anamtaka rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati ili kuokoa hali hiyo huku akitoa wito kwa tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC na  afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma kuchunguza miradi ya Tassia,Nyayo-Embakasi na hazina akidai uchunguzi wa awali wa bodi hiyo umebaini kasoro chungu nzima kwenye miradi hiyo.

Total Views: 383 ,