Athletico Madrid yaipiku Barca na Bayern ubora wa UEFA

Klabu ya Athletico Madrid chini ya ukufunzi wake diego Simeone imepanda katika orodha ya Uefa kama moja ya vilabu vilivyo bora zaidi katika dimba hilo na kuipiku klabu ya Barcelona na Bayern Munich ya ujerumani.

Kwenye orodha hiyo.. Real Madrid inaongoza ikiwa na alama 151, Athletico inafuata ikiwa na alama 133, Barca 128, Bayern Munich 122 , huku juve ikifunga 5 bora kwa alama 119.

Someone akijunga na klabu ya Athletico ilikuwa inashikilia nambari 23 lakini juhudi zake zimeimarisha klabu hiyo na kufanya vyema zaidi kwa kufika ngazi mbali mbali za juu katika dimba la Uefa.

Klabu inayoorodheshwa juu zaidi katika ligi kuu nchini uingereza ni klabu ya Mancity iliyo katika nafasi ya 9 na alama 94, Arsenal (11th – 84), Chelsea (13th – 80.363), Manchester United (16th – 78), Tottenham (22nd – 62.363) huku Liverpool ikiwa katika nafasi ya (35th – 44).

Total Views: 357 ,