Ashambuliwa Nyeti zake na Nyati Hola Kaunti ya Tana River

Mwanamume mmoja mjini Hola kaunti ya Tana River anaguza majeraha katika hospitali ya Hola baada ya kukatwa sehemu zake za siri baada ya kushambuliwa na Nyati.

Akithibitisha kisa hicho mkurugenzi wa shirika la huduma kwa wanyapori KWS John Wambua ameeleza kwamba mwanamume huyo kwa jina James Luli alikuwa akivua samaki pembezoni mwa mto Tana eneo la Malindi YA Ngwena kabla ya kushambuliwa.

Wambua aidha ametaja ongezeko la mizozo kati ya binadamu na wanyamapori huku akitoa onyo kwa wenyeji kutozuru maeneo yaliyo na wanyama hao kwa lengo la kulinda usalama wao huku akisema watakao patikana watakabiliwa kisheria.

Tayari uchunguzi umeanzishwa kubaini iwapo ni kweli mwanamume huyo alishambuliwa na Nyati kabla ya kuanza mchakato wa kumfidia.

Mwisho

Total Views: 306 ,