Asbel kuchuana na Centrowitt

Bingwa mara tatu wa dunia wa mbio za mita elfu moja na mia tano, Asbel Kiprop, anatarajiwa kuchuana na bingwa mpya wa michezo ya Olimpiki Matt Centrowitz, kwenye raundi ya kumi na moja na msururu wa mashindano ya “Diamond League” usiku huu , jijini Lausanne, Uswizi.

Asbel alimaliza katika nafasi ya sita kwenye michezo ya Olimpiki iliyomalizika hivi majuzi nchini Brazil, nyuma ya Centrowitz na atanuia kujiondolea fedheha nchini Uswizi.

Total Views: 327 ,