Asalimia 96 ya Shule za Msingi zapata umeme na vipakatalishi.

Mamlaka ya usambazaji umeme mashinani (REA) imetangaza kwamba asilimia 96 ya shule za msingi za umma zimepata umeme pamoja kupata vipakatalishi.

Mwenyekiti wa mamlaka hiyo Dkt.Simon Gicharu amesema shule elfu 23 tayari  zimeunganishwa  na mtandao wa umeme huku zaidi ya taasisi 250 zikitarajiwa kupata umeme katika miezi mitatu ijayo.

Kadhalika amedokeza kuwa kwa sasa wanakandarasi wako nyanjani kuhakikisha kwamba shughuli ya usambazaji wa vipakatalishi  kote nchini inafanikishwa.

Total Views: 436 ,