Akinyemi hatoshi asema Minaert

Kocha mkuu wa klabu ya Ingwee Ivan Minaaert amethibitisha kuwa huenda klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya kitaifa isimsajili mshambulizi tokea nigera Abass Akinyemi.

Mchezaji huyo amekuwa akifanya mazoezi na klabu hiyo kwa muda lakini Minaeert amehoji kuwa ni mchezaji mzuri ila mfumo wake itakuwa vigumu kuingiliana na jinsi anavyoifunza timu hiyo na kwamba haendani na sera zake za ukufunzi.

Ingwee tayari imewasajili wachezaji Harun Nyaka, Charles Bruno, Edwin Wafula, Ian Otieno Yusuf Suf, Jackson Saleh na Bernard Mang’oIi ambao tayari walishiriki katika nusu fainali za nane bora wikendi iliyopita.

Total Views: 367 ,