AK kuchagua kikosi cha chipukizi kwa riadha

Shirikisho la riadha nchini AK litakamilisha hii leo majaribio ya kuchagua timu itakayowakilisha taifa katika mashindano ya dunia ya IAAf kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 yanayoendelea katika uga wa nyayo zoezi liling’oa nanga hapo jana.

Mwenyekiti wa kamati ya michezo ya chipukizi AK Barnaba Korir amesema timu hiyo itawakilisha taifa katika mashindano ya IAAF yatakayofanyika mjini Bydgoszcz nchini Poland kati ya tarehe 19-24 mwezi ujao.

Huku hayo yakijiri ……. Sasa ni dhahiri kuwa wanariadha wa Kenya Pamoja na Urusi watafanyiwa ukaguzi binafsi wa kimatibabu na shirikisho la kukabiliana na utumizi wa dawa zilizoharamishwa kwa wachezaji ulimwenguni WADA kabla ya kuweza kushiriki mashindano ya olimpiki mjini Rio nchini Brazil.

Total Views: 390 ,