Ajuza wa 104, Atiwa nguvuni bila kosa

Ajuza mwenye umri wa miaka 104, anayeishi katika makazi ya wazee huko jijini Bristol Uingereza amekamatwa, kufungwa pingu, na kuwekwa kwenye gari la polisi na kuzungushwa mjini usiku kutwa.

Msikilizaji, si ati ajuza huyu alikuwa ametekeleza  uhalifu wowote bali alikuwa ametaka kutiwa nguvuni na polisi akiwa na umri wa miaka 104 kama moja wapo ya mapenzi yake akiwa kwenye makazi hayo ya wazee.

Inasemekana alikuwa ameandika kabisa azma hiyo  “ Ningependa nitiwe nguvuni nikifikisha umri wa  miaka 104, japo sijawahi kujipata pabaya na mkono wa sheria” Mwisho wa nukuu.

Baaadaye alisema kuwa alikuwa na siku njema na maafisa hao walioonekana tu wakizungumza naye lakini akasema amepata funzo la kuwa maakini na anacho kisema.

Picha: Kwa hisani

 

Total Views: 51 ,